Thursday 10 January 2013

NEW ZANZIBAR STARS INAREJEA KIVYENGINEEE......

KUNDI la miondoko ya taarab la New Zanzibar Stars limesukwa upya ili kuweza kupiga muziki wa ushindani.
 
New Zanzibar Stars ambalo katika miezi ya hivi karibuni, lilidorora na kupotea kwenye ushindani wa muziki, limeweka kambi yake Kawe jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Masae Garden View na litakuwa likitumbuiza ukumbini hapo kila Jumatano.

Mmoja wa viongozi wa kundi hilo, Rajab Kondo ambaye ni mahiri katika ucharazaji gitaa la bass, amewataka wale wote ambao walidhani New Zanzibar Stars imekufa, wafike kwa wingi Massae Garden, Jumatano hii (leo) na kila Jumatano ili wapate burudani iliyokwenda shule.

“Tumeisuka upya bendi yetu tukiwa na mseto wa wanamuziki chipukizi na wazoefu” alisema Kondo ambaye anasaidiwa na mpiga kinanda Ndagendage katika kuongoza jahazi la New Zanzibar Stars. 

Courtesy of Saluti5.....


1 comment:

  1. sasa hawa alipeana hati miliki kwa kundi la T moto kuiga nyimbo zao(zanzibar stars) hivi wao tena wataimba nyimbo gani!!!!!si itakua repeatation tu

    ReplyDelete