Wednesday 16 January 2013

MISAMBANOOOO ANASEMAJEEEE????......SHAABAN LAMANIA KIONGOZI NA MTUNZI WA EAST AFRICAN MELODY AFARIKI DUNIA.....

MWIMBAJI wa taarab na muziki wa dansi, Abdul Misambano “Super Rocks” amempongeza mkurugenzi wa Jahazi Modern Taarab, Mzee Yussuf kwa kuthubutu na hatimaye kufanikiwa kuunda kundi la Jahazi.
 
Misambano anayelitumikia kundi la TOT, aliyasema hayo alipokuwa anahojiwa na Hawa Hassan katika kipindi cha Sham Sham za Pwani cha ITV, Jumatatu usiku.


Alisema anampongeza kwa vile wako waimbaji wengi waliopata nafasi kama ya Mzee Yussuf lakini walishindwa kuzitimia.

Mwimbaji huyo aliyepata kutamba na wimbo wa “Asu” aliouimba akiwa na Babloom Modern Taarab, anamtaja Ali Hemed “Star” kama moja ya mifano yake.
 
“Enzi za Ali Star, nilishuhudia mwimbaji huyo akituzwa kapu la pesa, alikubalika sana na angeweza kabisa kuanzisha kundi lake na akafanikiwa lakini kwa bahati mbaya hakuthubutu.


“Mzee Yussuf alithubutu na akafanikiwa na pia ameweza kuzalisha wasanii nyota kama Isha Mashauzi na wengine wengi, kwahiyo nampongeza sana” alisema Misambano.



Misambano pia alishutumu tabia ya waimbaji wa sasa wa kiume kwa kuigana sana sauti kiasi cha kufikia hatua ya kushindwa kuwatofautisha.


“Zamani akiimba Misambano, Hussein Kibao, Ali Star, Mohamed Mrisho au Ali Taajiruna hutapata shida, kila mtu na sauti yake na staili yake.


Kizazi cha mwisho kukiona kikifanya kivyo ni Mzee Yussuf na marehemu Omar Kopa, walikuwa hawafanani, lakini baada ya hapo imekuwa taabu, ukimsikiliza Omar Teggo na Mzee Yussuf ni mle mle hakuna tofauti.


Huyu mtoto mpya wa Jahazi (Mohamed Ali) akiimba ni kule kule kwa Mzee, Amigo anajaribu kubadilika lakini bado kuna sehemu anapita pale pale kwa Mzee Yussuf, watu wanaigana sana” alisema Misambano.
Kundi la East African Melody
MKURUGENZI Mipango na mtunzi mkubwa wa nyimbo za kundi kongwe la East African Melody, Shaaban Lamania , amefariki alfajiri ya kuamkia leo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa fedha wa kundi hilo, Ashraf Mohamed, msiba uko Mbagala Kiburugwa, jijini Dar es Salaam.

Ashraf amesema mipango ya mazishi inaendelea na watatoa taarifa baadae kuhusu muda na siku ya mazishi.

Lamania ambaye amekuwa nje ya jukwaa kwa muda mrefu kutokana na ugonjwa wa kupooza, atakumbukwa kwa tungo zake nyingi ambazo hadi leo hii bado zinaendelea kulibeba kundi la Melody.

Miongoni mwa tungo zake kali ni pamoja na “Utalijua jiji” na “Mwanamke khulka”.

Mbali na utunzi, Lamania pia alikuwa mpigaji mahiri wa gitaa la solo.
‘Hakika sisi ni wa Mungu na kwake ni marejeo’.

Kwa hisani ya Saluti5...The screen masters..... 



No comments:

Post a Comment