
Thabit Abdul akiongoza mazoezi ya nyimbo mpya jana

Isha Mashauzi mazoezini jana

Aisha Othman Vuvuzela

Hashim Said "Mzee wa Majanga"

Jumanne Ulaya "J Four" akipiga gitaa la solo


Saida Mashauzi akiimba mazoezini jana

KUNDI la miondoko ya taarabu, Mashauzi Classic limekamilisha nyimbo mbili kati ya zitakazounda albam yao mpya ijayo.
Kuanzia
wiki iliyopita, kundi hilo lilianza rasmi mazoezi ya kutengeneza nyimbo
zao mpya na katika hali inayoonyesha uwezo mkubwa wa wasanii wao
kukamata nyimbo tayari vibao viwili “Mimi mwanaume” na “Ropokeni
yanayowahusu” vimekamilika.
Saluti5
ilitembelea mazoezi ya kundi hilo jana na kukuta nyimbo hizo zikiwa
katika hatua za mwisho kabla hawajaanza kugusa nyimbo nyingine.
Wimbo
“Mimi ni Mwanaume” umeimbwa na Hashim Said “Mzee wa Majanga” huku ule
wa “Ropokeni yanayowahusu” ukiimbwa na Aisha Othman “Vuvuzela”. Nyimbo
zote mbili ni utunzi wake Thabit Abdul.
Kwa hisani ya Saluti5....The screen masters.
twawasubiri na fujo lao
ReplyDelete