Mfalme Mzee Yussuf akizindua kibao chake 'Wasiwasi wako' |
Umati wa mashabiki uliohudhuria uzinduzi wa Jahazi juzi |
Waimbaji wa Jahazi wakiwa jukwaani tayari kwa uzinduzi |
Hawa Hassan wa ITV (kulia) A.K.A Toto la uhakika akiuliza swali maalum la kuzindua album |
Mwanne Othman A.K.A Toto la Matashtit wa East Africa Radio naye hakuachwa nyuma |
Mtangazaji wa Times FM, Ummy Suleiman ndani ya nyumba |
Mohamed Mauji akikamua gitaa la solo |
Mama kijacho, Malkia Leyla Rashid baada ya kumaliza kuimba wimbo wake mpya "Sitaki Shari" |
MABINGWA
wa mipasho, Jahazi Modern Taarab, usiku wa juzi walidhihirisha ubabe
wao kwenye muziki baada ya kuzindua kwa kishindo albamu yao mpya,
‘Wasiwasi Wako’.
Uzinduzi
huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Travertine Hotel, Magomeni, jijini Dar
es Salaam, kuanzia majira ya saa 4 usiku na kuendelea hadi usiku wa
manane.
Huwezi
kuamini, hadi saa 5 za usiku, tayari Jahazi walishavunja rekodi ya
mahudhurio ya makundi mengine yote yaliyowahi kuzindua kwenye ukumbi
huo.
Kiingilio cha sh. 20,000 hakikuwa kikwazo cha kuwazuia mashabiki pamoja na wapenzi kumiminika ukumbini humo na kujaa hadi kooni.
Kama ilivyotangazwa hapo awali, Jahazi walizindua albam yao bila kusindikizwa na msanii au kundi lolote lile.
Mzee
Yussuf ambaye juzi aliingia jukwaani bila mbwembwe zozote, aliwaachia
wapenzi fumbo moja: Aliuliza kama kuni inapikiwa, mwiko unafanyaje?
Na hayo yakijiri.....
Mzee Yussuf akiwa hospitalini jana jioni |
MASAA
machache kabla ya uzinduzi wa albam mpya ya Jahazi Modern Taarab,
mkurugenzi wa kundi hilo, Mzee Yussuf alilazwa kwa muda hospitalini
kufuatia malaria kali ilyompiga kwa takriban siku nne.
Mzee
Yussuf alilazwa hospital ya Mico Kinondoni ambako kwa siku zote hizo
nne alikuwa akienda hospitalini hapo na kulazwa muda wote wa mchana na
kisha jioni anaruhusiwa kwenda kulala nyumbani kwake.
Hali
hiyo ya ugonjwa, ilimfanya Mzee Yussuf atumbuize kwa shida jana usiku
na mara baada ya kumaliza kuimba wimbo wake ilibidi akapate mapumziko
mafupi.
Version yangu inakuja mda usiokuwa mrefu ila hii ni kwa hisani ya Saluti5 wa ukweee-eeh mtandao wa uhakika.
No comments:
Post a Comment