Thursday 24 January 2013

KHADIJA KOPA AINGIA STUDIO NA G FIVE....

MALKIA wa mipasho, Khadija Kopa, jana aliingia studio za Sofia Production ili kurekodi wimbo wake mpya wa taarab chini ya kundi la G Five.

G Five ambalo limeundwa na wasanii wa bendi tofauti kama vile TOT Taarab, Mashauzi Classic, Jahazi Modern Taarab, Five Stras na New Zanzibar Stars, limetengeneza jumla ya nyimbo sita.

Mkurugenzi wa kundi hilo Hamis Slim alisisitiza kuwa kundi hilo si bendi ya kudumu bali mkusanyiko wa muda na kisha kila mtu ataendelea na bendi yake.

Hata hivyo kazi ya kurekodi wimbo huo mpya wa Khadija Kopa uliopewa jina la “Fahari ya Mwanamke” haikukamilika kutokana na hitilafu ya umeme.

Kutokana na tatizo hilo, Khadija Kopa sasa atalazimika kumalizia kiporo cha kazi iliyobakia leo mchana. 

Kwa hisani ya Saluti5....The screen masters
 

No comments:

Post a Comment