Monday 7 January 2013

JOKHA AKIRI KUMCHAMBA LEILA RASHID........KASHESHEEEEE!!!

MWIMBAJI wa kundi la T-Moto Modern Taarab, Jokha Kassim, hatimaye amekiri kuwa anampiga vijembe mwimbaji wa Jahazi Modern Taarab, Leila Rashid.

Akiongea katika kipindi cha Hot Mix cha kituo cha televisheni cha EATV (Channel 5), Ijumaa iliyopita, Jokha alisema hata hivyo vijembe hivyo ni vya kibiashara.

Mwanzoni Jokha alikataa kabisa jambo hilo, lakini baada ya kubanwa sana na mtangazaji Mwanne Othman, hatimaye mwimbaji huyo, mke wa zamani wa Mzee Yussuf alikubali kuwa ndani ya nyimbo zake kuna vijembe vilivyolengwa kwa Leila Rashid.
 
Kwa muda mrefu sasa, Jokha ameonekana kama mtu wa kusubiria nyimbo za Leyla ambaye ni mke wa Mzee Yussuf na kisha kuzijibu.
Jokha Kassim (kushoto) akiwa na Mwanne katika studio za Channel 5
Katika wimbo Langu Rohoni wa Leila kuna mstari unasema “Si kama siwezi kusema, naweza mpaka kukesha” ambapo katika wimbo mpya wa Jokha Domo la Udaku utakutana na maneno “Kama kukesha kakesha popo, itakuwa wewe muokota makopo”.

Katika Sina Muda Huo wa Leila pale panaposema “Nina hamsini zangu zinanipeleka mbio”, Jokha anajibu tena katika Domo la udaku: “Huna hamsini wala mia”.

Kwenye wimbo mwingine wa Jokha, Unavyojidhani Hufanani, mwimbaji huyo anahoji: “Hicho cheo cha kujipachika alokupa ni nani” inaaminika ni kijiembe kwa Leila ambaye amekuwa akijulikana pia kwa jina la Malkia.

Courtesy of Saluti5....


1 comment: