HAKUWA
mtu wa makuu na inawezekana wengi wakawa hawafamu uwezo wake wala sura
yake …hakupenda kujikweza, lakini ni mtu mkubwa sana kwenye muziki wa
taarab pengine kuliko yeyote unayemdhania wewe.
Marehemu Lamania Shaaban
Huyo
ndie Lamania Shaaban aliyezikwa jana Tandika, Dar es Salaam huku
akisindikizwa na mamia ya wasanii, wadau, ndugu, jamaa na marafiki
waliopambwa na nyuso za huzuni.
Mwili wa Lamania aliyefariki juzi alfajiri ulipumzishwa katika nyumba yake ya milele majira ya saa saba za mchana.
Safari ya makaburini
Mwili wa Lamania Shaaban ukiingizwa kaburini
Mzee Yussuf ni kama haamini
Lamania
aliyezaliwa mwaka 1969, mwenyeji wa Zanzibar, alikuwa ndiye mkurugenzi
wa muziki wa East African Melody huku akiitungia zaidi ya nyimbo 40
ikiwa ni pamoja na kupanga mashairi na kutia sauti.
Lakini
pia hata nyimbo zilizotungwa na watu wengine bado zilipita kwenye
dawati lake na kuzifanyia uhariri. Alikuwa hana mpinzani katika gitaa la
solo ndani ya Melody.
Alijiunga na East African Melody mwaka 1994 na kuanzia hapo akawa ni moja ya mihimili mikubwa ndani ya kundi hilo.
Mkurugenzi mkuu wa East African Melody, Hajj Mohamed akihojiwa na Hawa Hassan wa ITV
Watoto wa Lamania Shaaban kutoka kushoto: Fatma, Mohamed, Nasria, Nasra na wa nyuma ni Shaaban
Wasanii
kama Mzee Yussuf, Hajj Mohamed, Khadija Kopa, Bi Mwanahawa Ali, Hassan
Soud, wote kwa nyakati tofauti waliiambia Saluti5 jana msibani kuwa
Lamania ni pengo kubwa katika muziki wa taarab ambalo litachukua muda
mrefu kuzibika.
Huku hayo yakijiri....MWIMBAJI
wa taraab wa Kings Modern Taarab, Hanifa Maulid, amsema licha ya kuvuna
elimu ya uimbaji lakini pia marehemu Lamania Shaaban amemwachia kumbu
kumbu kubwa.
Akiongea
na Saluti5 jana, Hanifa alisema alibahatika kuishi maisha ya ndoa na
Lamania ikiwa ni pamoja na kuzaa nae mtoto mmoja wa kike.
Enzi hizo marehemu Lamania na Hanifa Maulid
Hanifa Maulid akiwa na mtoto wake Nasra Lamania
Amesema
japo baadae aliachana na Lamania, lakini mtoto huyo Nasra Lamania ndiye
kumbukumbu pekee aliyoachiwa na mume wake huyo wa zamani.
Nasra
anayesoma darasa la kwanza anaungana na watoto wengine wanne wa Lamania
kutoka kwa mama mwingine kuunda jumla ya watoto watano waliachwa na
marehemu.
Kwa hisani ya saluti5...The screen masters.
No comments:
Post a Comment